Job 28:15-19

15 aHaiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi kuliko zote,
wala thamani yake haiwezi kupimwa kwa fedha.
16Haiwezi kununuliwa kwa dhahabu ya Ofiri,
kwa shohamu ya thamani kubwa au yakuti samawi ya thamani kubwa.
17 bDhahabu wala mawe maangavu haviwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi hubadilishwa na vito vya dhahabu.
18Marijani na yaspi hazistahili kutajwa;
thamani ya hekima ni zaidi ya akiki nyekundu.
19 cYakuti manjano ipatikanayo Kushi haiwezi kulinganishwa nayo,
wala haiwezi kununuliwa kwa dhahabu safi.
Copyright information for SwhNEN